Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 11:19

Cameroon yakata tiketi ya kwanza kuingia Nusu fainali


Mshambuliaji wa Cameroon Karl Toko Ekambi akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza wakati wa mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2021 kati ya Gambia na Cameroon kwenye Uwanja wa Japoma mjini Douala Januari 29, 2022. (Picha na CHARLY TRIBALLEAU).

Mataifa ya Timu ya taifa ya Cameroon Indimotible Lions imekuwa ya kwanza kukata tiketi ya kuingia nusu fainali baada ya kuibwaga Timu ya taifa ya Gambua Scor[pions kwa bao 2-0 katika mji wa Douala Jumamosi

Alikuwa ni mchezaji hatari wa Cameroon Karl Toko Ekambi anayechezea Lyon ya Ufaransa aliyepachika mabao yote mawili na kuipa ushindi muhimu nchi yake.

Cameroon walishambulia na kumiliki mchezo huo mwanzo hadi mwisho na kuwa njiani kurudia historia ya mwaka 2017 ya kuchukua kombe hilo ugenini lakini sasa wako nyumbani na wana nafasi nzuri zaidi.

Hata hivyo vijana wa Gambia wanarudi nyumbani wakiwa vifua mbele kwa kuweka historia ya kuingia kwa mara ya kwanza na kufika hatua kubwa ya robo fainali katika nchi yao.

Cameroon sasa wanangoja kupambana na mshindi kati ya Senegal na Equatorial Guinea watakaopambana kesho jumapili .

Karl Toko Ekambi wa Lyon ya Ufaransa amekuwa mshirika mkubwa wa mfungaji anayeongoza mpaka sasa katika michuano hiyo Vincent Abubakar kwa kufunga magoli matano huku Aboubakar akiwa na magoli 6.

Baadaye Jumamosi timu ya Burkinafaso inaingia uwanjani kupambana na Tunisia katika robo fainali ya pili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG