Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 11:34

Watu sita wafariki katika mkanyagano Cameroon


Watu wakiwasaidia waathiriwa wa mkanyagano nje ya uwanja wa ulikofanyika mchezo wa soka wa Kombe la Mataifa ya Afrika mjini Yaounde kati ya Cameroon na Comoro Jan. 24, 2022.

Takriban watu sita walifariki dunia katika mkanyagano nje ya uwanja katika mchezo wa soka wa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon, maafisa wamesema.

Mkanyagano huo ulitokea wakati umati wa watu ukihangaika kutaka kuingia katika uwanja wa Olembe katika mji mkuu, Yaounde, kutazama mchezo kati ya taimu ya taifa ya Cameroon na Comoro katika mechi ya mtoano wa 16 bora.

Mkuu wa mkoa, Naseri Paul Biya, alisema idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka, kwani hospitali katika eneo hilo iliripoti kuwa takriban watu 40 wamejeruhiwa katika mkanyagano huo.

"Baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya," alisema muuguzi Olinga Prudence.

"Tutalazimika kuwahamisha katika hospitali maalum." Maafisa walisema takriban watu 50,000 walijaribu kuhudhuria mechi hiyo.

Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu 60,000 lakini haukukusudiwa kujaa zaidi ya asilimia 80 kwa sababu ya vizuizi vya COVID.

Katika taarifa, Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF lilisema kwamba linafahamu tukio hilo kwenye Uwanja wa Olembe na linajaribu kupata maelezo zaidi juu ya kile kilichotokea.

Tunafanya mawasiliano ya mara kwa mara na serikali ya Cameroon na kamati ya maandalizi, CAF ilisema.

Leo usiku, Rais wa CAF Dkt Patrice Motsepe alimtuma katibu mkuu, Veron Mosengo-Omba, kuwatembelea mashabiki katika hospitali ya Yaounde iliongeza taarifa hiyo.

Klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Everton ilitoa heshima kwa wale waliopoteza maisha nje ya uwanja.

Katika ujumbe wa Twitter, klabu hiyo iliandika: "Mawazo na maombi ya kila mtu Everton yako pamoja na familia za mashabiki hao ambao wamepoteza maisha na yeyote aliyeguswa na matukio ya kusikitisha kwenye mechi ya leo ya #AFCON2021 kati ya Cameroon na Comoro mjini Yaounde. RIP.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG