Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:21

17 wafariki katika ajali ya moto Cameroon


Wapita njia wakiwapita polisi waliokuwa wakilinda lango la klabu ya usiku ya Livs ambapo moto mbaya ulitokea katika wilaya ya Bastos Yaounde, Jan. 23, 2022.
Wapita njia wakiwapita polisi waliokuwa wakilinda lango la klabu ya usiku ya Livs ambapo moto mbaya ulitokea katika wilaya ya Bastos Yaounde, Jan. 23, 2022.

Cameroon inasema imefungua uchunguzi kufahamu majina na utaifa wa watu 17 waliofariki Jumapili katika moto uliosababishwa na mlipuko katika mji mkuu Yaounde.

Mlipuko uliotokea katika klabu maarufu ya usiku pia umejeruhi watu wanane. Serikali imewataka watu kuwa na utulivu wakati maelfu ya mashabiki wa kandanda wako mjini Yaounde kwa mashindano yanayoendelea la kombe la mataifa ya Afrika (AFCON).

Mamia ya watu wakiwemo maafisa wa serikalli ya Cameroon walijitokeza huko Bastos, kwenye ujirani uliopo mjini Yaounde, Jumapili asubuhi. Waliwaangalia jinsi majirani na wafanyakazia wa Livs, klabu maarufu ya usiku, na kikosi cha kijeshi cha zimamoto cha Cameroon, wakipekua kwenye majengo yaliyoungua katika eneo hilo.

Miongoni mwa raia waliojishughulisha na kusaidia kuwatafuta majeruhi alikuwa Gustav Lemaleu mwenye umri wa miaka 27. Lemaleo anasema raia na idara ya zimamoto wamewaokoa kiasi cha watu 40. Anasema ni vigumu kufahamu majina na utaifa wa wale waliojeruhiwa na waliokufa kwasababu wateja huwa hawatakiwi kuonyesha vitambulishe kabla ya kuingia Livs.

Lemaleu amesema ana uhakika kwamba baadhi ya waathirika ni pamoja na watu ambao wanaitembelea Cameroon kujionea michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini humo.

Katika taarifa, serikali inasema ajali ya moto kwenye klabu ya usiku ilisambaa hadi kwenye duka la kuuza gesi ya kupikia. Milipuko mikubwa ilisikika kutoka kwenye mitungi ya gesi sita, na kusababisha taharuki kubwa katika ujirani huo.

Waziri wa Afya ya Umma, Manaouda Malachie anasema Rais Paul Biya alijulishwa juu ya tukio hilo mara tu lililpotokea. Manaouda anasema Biya ameamuru wafanyakazi wa afya kuwasafirisha majeruhi kwenye hospitali kuu ya Yaounde.

Anasema Biya ameiomba wizara ya afya ya umma kuwatibu majeruhi bila ya kudai malipo na kwamba mipango inafanywa kwa waliofariki kuzikwa katika maeneo yao ya asili baada ya uchunguzi. Anasema Biya ameiamuru wizara hiyo kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wanafamilia ambao wamepata kiwewe hasa pale wanapowatambua jamaa zao.

Rene Emmanuel Sadi, Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon, alitembelea eneo la ajali. Anasema ni mapema mno kufahamu majina na nchi wanazotokea wale waliofariki na kujeruhiwa.

Sadi anasema “bado tuko katika kiwango cha uchunguzi. Tukio ni kubwa sana. Kuna watu ambao wamefariki. Wengine wamejeruhiwa na uchunguzi unaendelea. Nadhani wakati mambo yote haya yatakapokwisha, nitawapa habari za uhakika kuhusiana na tukio hilo baya sana.”

Sadi amesema idadi ya vifo huenda ikaongezeka.

Rais Paul Biya ameomba kuwepo kwa utlivu na kuwahakikishia usalama wachezaji, mashabiki na maafisa wa michezo wanaohudhuria mashindano ya AFCON mjini Yaounde.

Cameroon ni mwenyeji wa maelfu ya watu wanaohudhuria michuano hiyo, ambayo ilianza Januari 9 na itamalizika Februari 6.

XS
SM
MD
LG