Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:40

Mashabiki 1,500 wa kandanda wawasili Cameroon kuunga mkono timu zao


Ramani ya Cameroon na majirani zake Equatorial Guinea na Gabon.
Ramani ya Cameroon na majirani zake Equatorial Guinea na Gabon.

Cameroon inasema kwamba ndani ya siku nne, kiasi cha mashabiki 1,500 wa kandanda wameingia nchini kutoka nchi jirani za Equatorial Guinea na Gabon kuziunga mkono timu zao ambazo zimesonga mbele katika raundi ya 16 bora katika michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika – AFCON.

Gabon inapambana Jumapili na Burkina Faso wakati Equatorial Guinea itacheza dhidi ya Mali siku ya Jumatano. Waandaaji wa mashindano hayo wanataka mashabiki wote kupimwa COVID-19 kabla ya kuingia uwanjani.

Mashabiki wa Gabon
Mashabiki wa Gabon

Polisi wa uhamiaji nchini Cameroon walisema Jumamosi kwamba mabasi yaliyobeba takriban mashabiki 900 wa kandanda kutoka Gabon na Equatorial gunea wamengia katika taifa hilo la Afrika ya Kati ndani ya saa 48. Gabon na Equatorial gunea ni majirani wa Cameroon upande wa Kusini.

Polisi wa uhamiaji wamesema kiasi cha mashabiki 600 kutoka Gabon na Equatorial Guinea waliwasili nchini Cameroon kwa usafiri wa bahari na wengine kwa kutumia usafiri wa ndege.

Cameroon inasema mmiminiko huo umekuja baada ya Gabon na Equatorial Guinea kufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano katika mashindano ya AFCON, nchini Cameroon. Gabon ilipata sare ya 2 -2 siku ya Jumanne dhidi ya Morocco mjini Yaounde, timu zote mbili zimesonga mbele.

Mashabiki wa Equatorial Guinea
Mashabiki wa Equatorial Guinea

Equatorial Guinea ilijihakikisha nafasi baada ya ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Sierra Leone katika mechi za makundi ambapo ilicheza katika uwanja wa Limbes Omnisport upande wa kusini magharibi nchini humo ambako wanatumia lugha ya kiingereza.

Prosper Ebang mwenye umri wa miaka 30 ni miongoni mwa mashabiki kutoka Gabon na Equatorial Guinea, polisi wa Cameroon wanasema wameingia nchini humo. Ebang anasema anataka kuwa sehemu ya tukio ya kandanda ambako timu ya taifa ya nchi yake, Panthers of Gabon inafanya vzuri.

Ebang anasema hakuna raia ambaye anaipenda Gabon anaweza kuwa tofauti wakati Panthers inaipofanya Gabon kujivuna kwa kandanda safi ambayo wameionyesha nchini Cameroon wakati wa AFCON. Anasema ana uhakika kwamba Gabon itafika katika fainali za AFCON kama Cameroon itaendelea kutoa mazingira mazuri kwa michezo.

Felix Nguele Nguele ni gavana wa mkoa wa kusini nchini Cameroon ambao unapakana na Gabon na Equatorial Guinea. Anasema maafisa wa Gabon na Equatorial Guinea wamemjulisha kwamba mamia ya mashabiki bado wako njiani kuelekea Cameroon.

Nguele anasema amewaomba polisi na jeshi upande wa kusiniwa mpaka huko Cameroon kuhakikisha usalama wa mashabiki wa kandanda kutoka Gabon na Equatorial Guinea. Anasema anafahamu kwamba watu mara nyingine wanakuwa na nia ambazo si nzuri na huenda wakata kuwabughudhi mashabiki kutoka nje ya nchi kwa vile mivutano imeongezeka kati ya Cameroon na Equatorial Guinea tangu mwezi Novemba.

Novemba 30, 2021, Cameroon ilisema Equatorial Guinea ilikuwa ikiwafukuza maelfu ya raia wa Cameroon ambao walikuwa wakiishi katika nchi hiyo jirani kinyume cha sheria, na kuelezea wasi wasi wa usalama. Maafisa katika mji mkuu, Malabo, alisema raia wa Cameroon wamekimbia mzozo upande wa magharibi mwa nchi yao, ambako wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipambana na wapiganaji wanaotaka kujitenga wanaotumia lugha ya kiingereza.

Kanda za video kutoka wananchi wa Cameroon waliofukuza Equatorial guinea zilifurika kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na WhatsApp.

Kisito Esuarais wa taasisi isiyo ya kiserikali ya South West Youth league, yenye makao yake Limbe, mji wa kusini magharibi unaotumia lugha ya kiingereza, anasema taasisi yake inawapatia mafunzo vijana kuwa wakarimu kwa mashabiki wanaofika nchini Cameroon kuziunga mkono timu zao za kandanda.

“Mmiminiko wa mashabiki na wafuasi kutoka Gabon na Equatorial Guinea ni mkubwa sana. Mashabiki wamekuwa wakija kwa idadi kubwa kwa njia ya ndege, ardhi na majini, tunadhani watu wengi watafika kuangalia kandanda. Kwahiyo tumehakikisha kwamba mazingira ni rafiki, na yanayofaa,” amesema Esua.

Wizara ya afya ya umma ya Cameroon inasema mashabiki ambao wamewasili ndani ya saa 48 zilizopita lazima wahesimu miongozo ya masharti ya Covid 19 yaliyowekwa na Shirikisho la Kandanda Afrika(CAF). CAF inasema watu lazima wawe na majibu ambayo yanaonyesha hawana Covid 19 vipimo ambavyo vimechukuliwa ndani ya saa 24 pamoja na uthibitisho kuwa wamepatiwa chanjo dhidi ya Covid 19 ili kupata fursa ya kuingia viwanjani kwa michezo ya AFCON.

Balozi Gabon na Equatorial Guinea mjin Yaounde zinasema mashabiki wote wanaoingia nchini humo lazima waheshimu sheria za Cameroon na masharti ya Covid 19 yaliyowekwa na Cameroon na CAF kwa muda wote watakaouwa nchini humo.

XS
SM
MD
LG