Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:21

Bunge la Peru laidhinisha mpango wa kuitisha uchaguzi mapema


Bunge la Peru
Bunge la Peru

Bunge la Peru limeidhinisha mpango wa kuitisha uchaguzi wa mapema katika jaribio la kuzima mzozo wa siasa kitaifa ambao ulipelekea ghasia mbaya sana baada ya wabunge kumuondoa mamlakani Rais Pedro Castillo

Rais wa Peru Pedro Castillo aliyeondolewa madarakani akijaribu kulivunja bunge.
Rais wa Peru Pedro Castillo aliyeondolewa madarakani akijaribu kulivunja bunge.

Pendekezo hilo limeidhinishwa na wabunge 91 kati ya wanachama 130 katika bunge hilo, na huenda likausukuma uchaguzi hadi Aprili 2023 kwa ajili ya rais na bunge ambapo awali uchaguzi ulipangwa kufanyika mwaka 2026.

Mpango huu lazima uidhinishwe na duru nyingine ya wingi wa theluthi mbili kwa hatua hiyo kupitishwa rasmi.

Hatua hiyo imeungwa mkono na rais wa muda Dina Boluarte, ambaye alichukua madaraka kutoka kwa Castillo baada ya mwalimu wa shule wa zamani kujaribu kulivunja bunge hapo Desemba 7.

Baada ya kushindwa katika hatua hiyo, Castillo alikamatwa.

XS
SM
MD
LG