Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:42

Hali ya tahadhari imetangazwa Peru, rais wa zamani anazuiliwa gerezani


Polisi wakikabiliana na wafuasi wa aliyekuwa rais wa Peru aliyeondolewa madarakani Pedro Castillo. Dec 14,2022
Polisi wakikabiliana na wafuasi wa aliyekuwa rais wa Peru aliyeondolewa madarakani Pedro Castillo. Dec 14,2022

Serikali ya Peru imetangaza siku 30 za hali ya dharura kufuatia maandamano mabaya baada ya rais Pedro Castillo kuondolewa madarakani.

Rais mpya wa Peru Dina Boluarte, amewataka raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na kuonyesha nia ya kuandaa uchaguzi mkuu katika muda wa mwaka mmoja.

Waandamanaji wanataka uchaguzi mkuu kufanyika mara moja kumchagua rais na wabunge.

Castillo anazuiliwa gerezani huku maafisa wakitayarisha keshi ya mapinduzi dhidi yake.

Waziri wa ulinzi Luis Otarola Penaranda ametangaza kwamba polisi wa kitaifa na jeshi la nchi hiyo watahakikisha kwamba kuna hali ya utulivu na kulinda mali ya umma kote nchini humo.

Castillo aliondolewa madarakani December 7 alipojaribu kuvunja bunge lililokuwa linatayarisha mswaada wa kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye.

Alikamatwa katika barabara za Lima akiwa pamoja na walinzi wake, na waendesha mashtaka wanasema alikuwa anajaribu kutorokea nchini Mexico.

XS
SM
MD
LG