Kwenye hatua iliyolitikisa taifa, wabunge walipiga kura ya kumuondoa Castillo kufuatia jaribio lake la kujitwika madaraka yote na kuvunja bunge kabla ya kupigwa kwa kura ya kutokuwa na Imani naye.
Hatua hiyo inaonekana kuwa mwendelezo wa kuyumba kwa kisiasa, kwa kuwa marais watano ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita wameshindwa kumaliza muda wao .
Castillo ambaye alikuwa mwalimu na kiongozi wa wafanyakazi alishinda kwa kura chache 2021 kupitia wapiga kura masikini kutoka maeneo ya vijijini, na alikamatwa Jumatano kwa tuhuma za ukatili pamoja na ufisadi.