Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 14:11

Bunge la Marekani laidhinisha kikomo cha ongezeko la deni la taifa


Mfano wa dola ya Marekani
Mfano wa dola ya Marekani

Baraza la Wawakilishi lilipitisha kikomo cha ongezeko la deni, mapema Jumatano kwa kura 221 kwa 209 na kura moja pekee ya Republican iliyounga mkono.

Uidhinishaji wa Seneti ulikuja Jumanne kwa kupitishwa na Wademocrat 50 kwa kura ya “Ndio” huku Warepulikan 49 wakipinga.

Bunge la Marekani limeidhinisha hatua ya kuongeza kiwango cha deni la taifa na kupigia kura ili kuepuka kushindwa kulipa deni. Rais Joe Biden bado anahitaji kutia saini sheria hiyo hatua ya mwisho katika mchakato huo ambao umewagawa waDemocrats na waRepublicans kwa miezi kadhaa.

Baraza la wawakilishi lilipitisha kikomo cha ongezeko la deni, mapema leo jumatano kwa kura 221 kwa 209 na kura moja pekee ya Republican iliyounga mkono. Uidhinishaji wa seneti ulikuja Jumanne kwa waDemocratic 50 kupiga kura ya “Ndio” na waRepuplican 49 wakipinga.

Waziri wa fedha Marekani, Janet Yellen
Waziri wa fedha Marekani, Janet Yellen

Waziri wa fedha Marekani, Janet Yellen aliwaonya wabunge kwamba wizara yake inaweza kuachwa bila fedha za kutosha kufadhili shughuli za serikali kuanzia mapema Jumatano.

Sheria hiyo inaongeza kikomo cha deni kwa dola trilioni 2.5 ambapo kiongozi wa walio wengi katika seneti Chuck Schumer alisema ingeruhusu kufadhili majukumu ya serikali kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwaka 2022 hadi 2023.

XS
SM
MD
LG