Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:56

Uharibifu mkubwa na vifo vyaendelea kuripotiwa Marekani kutokana na Dhoruba kali


Kituo cha kusambaza mizigo kutoka Amazon kilichoharibiwa na dhoruba
Kituo cha kusambaza mizigo kutoka Amazon kilichoharibiwa na dhoruba

Wakaazi wa kaunti za Kentucky ambako dhoruba kali iliua darzeni ya watu huenda wakakosa umeme na maji  kwa  wiki kadhaa au hata zaidi huku viwango vya baridi vikiendelea kuongezeka.

Dhoruba hiyo ilisababisha uharibifu mkubwa na vifo vya watu kadhaa katika majimbo Matano ya Marekani mwishoni mwa wiki.

Maafisa katika jimbo la Kentucky wamesema kwamba uharibifu mkubwa uliotokea unatatiza uwezo wa kuthathimini hali halisi iliyosababishwa na Dhoruba hiyo kali iliyotokea ijumaa.

Watu 88, wakiwemo 74 katika jimbo la Kentucky walifariki kutokana na dhoruba hiyo iliyoharibu nyumba ya kuwahudumia watu wazee katika jimbo la Arkansas, kituo cha kusambaza bidhaa za Amazon katika jimbo la Illinoi.

Uharibifu mkubwa pia ulitokea katika majimbo ya Tennessee na Missouri.

Shughuli ya kuwatafuta watu ambao hadi sasa hawajulikani walipo inaendelea.

Maafisa pia wanafanya kila juhudi kurejesha umeme huku wakitoa msaada wa chakula na maji kwa waathirika ambao wamepewa makazi mbadala.

"Wakaazi 109 wa Kentucky hawajulikani walipo, lakini ninapotazama uharibifu uliotokea, watu wengi hawajulikani walipo. 81 kati yao wapo katika kaunti ya Hopkins pekee. 22 katika kaunti ya Waren, watano katika kaunti ya Graves, na hiyo si sawa. Kuna wengi zaidi ya hao tunaostahili kuwatambua na kuwapata tukiwa na matumanini kwamba wapo salama na hai. Kwa sababu nyumba kadhaa ziliharibiwa, juhudi za uokoaji huenda zikatekelezwa pole pole lakini tutafanya kila tuwezalo kutoa taarifa za uhakika." amesema Gavana Andy Beshear wa Kentucky.

Idadi kubwa ya watu ambao hawajulikani walipo wapo katika kaunti ya Dawson, mji mdogo wenye wakazi karibu 3,000.

Wakaazi wana kumbukumbu ya kilichotokea wakati dhoruba ilipopiga.

"Kulikuwa na upepeo mkali sana. tulidhani ilikuwa ni dhoruba ya kawaida. Lakini mara hii, ilikuwa kali sana. nakumbuka baba yangu akipaza sauti na kusema twende katika vyumba vya chini ya nyumba katika sehemu salama. Nilisikia sauti kubwa na vitu vikivunjika. Dada yangu alikuwa akilia, aliogopa sana. hii ndio mara ya kwanza nimekuja hapa kuona uharibifu uliotokea. Ni vigumu kuamini kwamba huu ni mji wangu." amesema mkaazi wa Elektra.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba atakwenda Kentucky kesho jumatano, jimbo ambalo limepata uharibifu mkubwa kati ya majimbo manane ambayo dhoruba hiyo ilipiga.

XS
SM
MD
LG