Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 05:05

Biden na mkewe Jill wawasili London kuhudhuria mazishi ya Malkia


Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Stansted London, huko Stansted, Uingereza, Sept. 17, 2022.

Biden, ambaye aliwasili siku ya Jumamosi, ni kati ya mamia ya viongozi wa dunia waliokusanyika Uingereza kuhudhuria mazishi ya malkia Jumatatu.

Biden na mkewe wanatarajiwa kutoa heshima zao za mwisho kwa Elizabeth Jumapili huko katika Ukumbi wa Westminster, ambapo mwili wake umewekwa tangu Jumatano, ili kuwapa watu fursa ya kutoa heshima zao.

Familia za wafalme kutoka nchi mbali mbali za Ulaya pia wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya maziko ya Elizabeth.

Mfalme Charles III, mtoto wa Elizabeth, anaandaa tafrija rasmi ya kitaifa Jumapili kwa ajili ya viongozi mbalimbali ambao wamekusanyika katika mji mkuu wa Uingereza.

Ufalme wa Uingereza umetoa mwaliko unaozusha utata kwa mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman, ili kuhudhuria mazishi, mtu ambaye inaaminika na wengi kuwa alihusika na amri ya kuuawa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi mwaka 2018.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG