Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:48

Biden kutembelea eneo la mpakani kati ya Poland na Ukraine


Rais Joe Biden akipanda ndege kuelekea Poland
Rais Joe Biden akipanda ndege kuelekea Poland

Rais wa Marekani,  Joe Biden, Ijumaa atatembelea mji wa Poland, ambao uko karibu na mpaka na Ukraine, kwa lengo la kuonyesha ushirikiano  na Ukraine ambayo inavamiwa na Russia, White House imesema.

Biden atatembelea eneo la Rzesow, lililo umbali wa kilometa 50 kutoka mpakani mwa Ukraine, ambako anatarajiwa kukutana na Rais wa Poland, Andrzej Duda.

Ni sehemu ya safari yake ya dharura barani Ulaya ambayo imesababiswha na vita vya Ukraine, ambapo pia ameshiriki mikutano kasha nchi Ubelgiji.

Akiwa nchini Poland, Bidenpia atapokea taarifa ya namna gani nchi hiyo inakabiliana na wimbi la mamilioni ya wakimbizi, ambao wanakimbia makombora ya Russia nchini Ukraine.

Rais huyo pia atakutana na wanajeshi wa kikosi cha anga ambao wana kambi yao katika eneo hilo la Rzeszw.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya umeishutumu Russia, kwa kile ulichokiita “uhalifu wa kivita chini Ukraine.”

Azimio la viongozi wa Umoja huo, baada ya mkutano wao mkuu mjini Brussels, Ubelgiji, linasema serikali ya Russia itawajibishwa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Baraza la Ulaya limesema kuwa Russia imekuwa ikitekeleza mashambulizi dhidi ya umma, na kuyalenga maeneo ya watu, ikiwa ni Pamoja na hospitali, viwanda vya dawa, shule na makazi.

XS
SM
MD
LG