Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:38

Biden aelekea Ulaya kuungana na viongozi wengine kutafuta suluhu mzozo wa Ukraine


Rais wa Marekani Joe Biden   REUTERS/Leah Millis
Rais wa Marekani Joe Biden   REUTERS/Leah Millis

Rais wa Marekani Joe Biden ameondoka Washington saa chache zilizopita akielekea Ulaya wakati vita vya Ukraine vikiripotiwa kufikia hatua  muhimu sana.

Rais wa Marekani Joe Biden ameondoka Washington saa chache zilizopita akielekea Ulaya wakati vita vya Ukraine vikiripotiwa kufikia hatua muhimu sana.

Bidena anatarajiwa kukutana na washirika muhimu wa Marekani, mjini Brussels na Warsaw, wiki hii wakati viongozi wanajaribu kuzuia vita vya Russia dhidi ya Ukraine kusambaa zaidi.

Ziara ya Biden ya siku nne, ni mtihani kwa uwezo wake wa kumaliza mgogoro mbaya zaidi kutokea Ulaya tangu vita vya pili vya Dunia vilivyomalizika mwaka 1945.

Kuna wasiwasi kwamba huenda Russia ikatumia silaha za kemikali au nuclear katika uvamizi wake nchini Ukraine, unaoripotiwa kukwama kwa sasa kutokana na matatizo ya kiufundi na upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine.

Akiondoka White house, Biden amesema kwamba kuna tishio la uhakika kwamba Russia inaweza kutumia silaha hizo.

Mamilioni ya watu wamekimbia Ukraine, wengi wao wakiingia nchini Poland.

XS
SM
MD
LG