Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 19:08

Rais wa Marekani Joe Biden kuzungumza na rais wa China, Xi Jing Ping


Rais wa Marekani, Joe Bide, ambaye yupo katika mazungumzo na rais wa China, Xi Jingping (Picha na REUTERS/Leah Mills)

Washington imeelekeza nguvu zake Beijing, Alhamisi, ambapo rais wa Marekani, Joe Biden, alipanga kufanya mazungumzo ya nadra na rais wa China, Xi Jinping.

Mazungumzo hayo yanakuja wakati rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy akiomba dunia imsaidie kupambana na uvamizi wa Russia wa wiki tatu sasa.

Nafasi muhimu ya China inaongezeka katika mgogoro kufuatia ripoti kwamba Russia imeomba msaada wa kijeshi kwa China.

Marekani inatoa fungu la msaada wa kijeshi kwa Ukraine, huku Biden akitangaza msaada mwingine wa dola milioni 800 kwa ajili ya ulinzi wiki hii.

Msemaji wa White House, Jen Psaki amesema kwamba wameweka wazi kuhusu wasiwasi mkubwa waliokuwa nao kuhusu China kuiunga mkono Russia na uwezekano wa yale yanayoweza kujitokeza.

Psaki amesema kwamba mazungumzo hayo ya simu yatakuwa muhimu kwa rais Biden kufanya tathimini msimamo wa rais wa China, Xi Jingping.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG