Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 21:29

Biden asema Marekani iko macho kuhakikisha Septemba 11 haitokei tena


Watu wahudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya shambulizi la kigaidi la Septemba 11, huko New York.

Katika maadhimisho ya miaka 21 ya mashambulizi ya September 11 hapa nchini Marekani, Wamarekani walikusanyika kuadhimisha tarehe hiyo na kuwakumbuka wale waliopoteza maisha.

Rais Joe Biden aliweka shada la maua jana Jumapili huko Pentagon, nje kidogo ya Washington, ambako watu 184 waliuawa wakati ndege iliyotekwa nyara ilipopiga kwenye jengo hilo.

Rais Biden
Rais Biden

Rais alikiri kuwa majonzi waliyopata familia za wale waliopoteza maisha na kuahidi kuiweka Marekani katika hali ya tahadhari dhidi ya mashambulizi yoyote mengine.Rais Biden alieleza: “Hakuna gaidi anaigusa nguvu ya Marekani ni juu yetu kuiweka salama kwa niaba ya wale wote ambao wamepoteza maisha miaka 21 iliyopita. Kwa niaba ya wale wote ambao walijitolea nafsi zao kwa taifa hili kila siku tangu siku hiyo. Hiyo ni kazi yetu sote.”

Huko New York, Makamu Rais Kamala Harris na mume wake Dough Emhoff, walihudhuria sherehe kwenye eneo la kumbukumbu mahali ambako yalikuwepo majengo pacha ya World rade Center wakati huo.

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na mumewe Doug Emhoff akizungumza na kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer na Gavana wa New York Kathy Hochul katika kumbukumbu ya Septemba 11, Jumapili, 2022, New York.AP Photo/Julia Nikhinson)
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris na mumewe Doug Emhoff akizungumza na kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer na Gavana wa New York Kathy Hochul katika kumbukumbu ya Septemba 11, Jumapili, 2022, New York.AP Photo/Julia Nikhinson)

Familia zilisoma kwa sauti majina ya waathirika, wakinyama kwa muda saa ambayo ndege ziliyapiga majengo hayo mawili na kusababisha vifo vya takriban watu elfu tatu.

Michael mume wake Diane Massaroli, alikuwa akifanya kazi kwenye ghorofa ya 101 katika eneo North Tower.

Diane Massaroli, Mjane wa Septemba 11 anaeleza: “Ah, alikuwa mtu mzuri sana, baba mwema, mume mzuri, mfanyakazi hodari, alipenda mchezo wa bowl, alikuwa mtu wa aina yake. Ndiyo maana kila mwaka nakuja hapa na kubeba picha yake. Hata watu ambao hawajawahi kumfahamu wanamjua na kukumbuka sura yake kwasababu alikuwa na maisha yenye thamani.”

Katika kumbukumbu ya Kitaifa ya Ndege namba 93 huko Shanksville, Pennyslvania, mke wa rais Jill Biden, aliwakumbuka abiria wa ndege hiyo ambao waliiangusha ndege iliyokuwa imetekwa na kuvuruga azma ya shambulizi kuja Washington.

Jill Biden, Mke wa Rais alikuwa na haya ya kusema: “Kama tulivyo simama katika ardhi hii takatifu na yenye makovu, rekodi ya majonzi yetu sote, na kumbukumbu ambazo tunaishi nazo hadi hivi leo. Hili ni jamboa ambalo tutakuwa nalo siku zote. Matumaini yataishinda chuki. Mapenzi yataishinda hasara. Na uhusiano ambao utatuweka pamoja katika yote haya.”
Jamii nyingine kotenchini zilifanya kumbumbuku zao ikiwa ni pamoja na kuwasha mishumaa, huduma za kidini na kumbukumbu nyingine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG