Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:28

Biden akutana na Rais wa Poland na wakimbizi wa Ukraine mjini Warsaw

Rais wa Marekani Joe Biden akimsalimia mtoto katika kundi la wakimbizi wa Ukrainian huko kwenye Uwanja wa Taifa wa PGE Warsaw, Poland Machi 26, 2022. REUTERS/Evelyn Hockstein
Rais wa Marekani Joe Biden akimsalimia mtoto katika kundi la wakimbizi wa Ukrainian huko kwenye Uwanja wa Taifa wa PGE Warsaw, Poland Machi 26, 2022. REUTERS/Evelyn Hockstein

Poland, mwanachama wa NATO, amepokea zaidi ya wakimbizi wa Ukraine milioni 2. Biden, akiwa amefuatana na Meya wa Warsaw Rafal Trzaskowski anatarajiwa kukutana na baadhi ya wakimbizi Jumamosi kujadili juhudi za kuwapatia misaada ya kibinadamu.

Rais wa Marekani Joe Biden yuko Warsaw Jumamosi, ambako atakutana na Rais wa Poland Andrzej Duda na maafisa wengine wa Poland kujadili uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Mkutano huo unafanyika, Marekani imesema, wakati ambapo Russia inaelekea kubadilisha mwelekeo wake wa mashambulizi ya kijeshi kutoka mji mkuu wa Ukraine, Kyiv kugeukia mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mwenyeji wake Rais wa Poland Andrzej Duda akikagua gwaride la heshima kabla ya kuanza mkutano wao nje ya Kasri ya Rais, Warsaw, Poland Machi 26, 2022.Slawomir Kaminski /Agencja Wyborcza.pl via REUTERS
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na mwenyeji wake Rais wa Poland Andrzej Duda akikagua gwaride la heshima kabla ya kuanza mkutano wao nje ya Kasri ya Rais, Warsaw, Poland Machi 26, 2022.Slawomir Kaminski /Agencja Wyborcza.pl via REUTERS

Poland, mwanachama wa NATO, amepokea zaidi ya wakimbizi wa Ukraine milioni 2. Biden, akiwa amefuatana na Meya wa Warsaw Rafal Trzaskowski anatarajiwa kukutana na baadhi ya wakimbizi Jumamosi kujadili juhudi za kuwapatia misaada ya kibinadamu.

Baadae siku ya Jumamosi, Biden atatoa hotuba katika Kasri ya Kifalme ya Warsaw kuhusu “hatari za wakati huu,’ kulingana na mshauri wa usalama wa kitaifa Jake Sullivan.

Akiwa Poland Ijumaa, Biden aliipongeza Poland kwa kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi na kukutana na watoa huduma za kibinadamu wa Poland na majeshi ya Marekani yaliyoko karibu na mpaka wa Ukraine.

“Nyinyi mpo katikati ya mapambano kati ya demokrasia na ukandamizaji,” Biden alisema wakati akikutana na Jeshi la Marekani la Kikosi cha Airborne 82 huko Rzeszow, ambacho kinawasaidia maelfu ya vikosi vingine vya NATO huko katika nchi zilizoko upande wa mashariki ikiwemo Poland, Lithuania, Latvia, Estonia, Bulgaria na Romania.

Ziara ya kwanza ya Biden kukutana na wanajeshi wa Marekani huko Poland Ijumaa ilikuwa katika duka la kinyozi la muda kwenye makao makuu ya muda ya kikosi hicho. Baadae alisimama katika jengo ambalo wanajeshi wanapata mlo wao, ambapo alikaa na kushiriki kula nao pizza.

“Nyinyi ndio wapiganaji mahiri zaidi duniani na hiyo siyo hyperbole,” Biden alisema kabla ya kukaa na wanajeshi hao kula nao.

Rais Joe Biden akiwa na wanajeshi wa Marekani alipowatembelea katika Kikosi chao karibu na mpakani mwa Ukraine, Jasionka, Poland. (AP Photo/Evan Vucci)
Rais Joe Biden akiwa na wanajeshi wa Marekani alipowatembelea katika Kikosi chao karibu na mpakani mwa Ukraine, Jasionka, Poland. (AP Photo/Evan Vucci)

Mabadiliko ya mkakati

Ukilinganisha pande hizo mbili, maafisa wa Marekani na nchi za Magharibi wamesema pamoja na idadi kubwa, wanajeshi wa Russia wameendelea kuhangaika huko Ukraine, ikiwalazimu kubadilisha mkakati.

“Tunafikiria wanajaribu kulizingira eneo la Donbas,” afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la ulinzi la Marekani amewaambia waandishi wa habari, akizungumza kwa sharti kwamba jina lake lisitajwe ili aweze kujadili masuala ya kijasusi.

“Tumekuwa tunalizungumzia hili kwa wiki kadhaa hivi sasa,” afisa huyo amesema kuhusu kubadilika kwa vipaumbele vya jeshi la Moscow.

“Hapo ndipo bado kuna mapambano makali sana, na tunafikiria wanajaribu siyo tu kudhibiti kwa kiwango fulani eneo kubwa kama ni mbinu ya kupata uzito katika meza ya mashauriano, lakini pia kuyazuia majeshi ya Ukraine yabakie upande wa mashariki ya nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG