Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:25

Jaji Ketanji anaendelea kujitetea katika kamati ya seneti


Jaji Ketanji Brown Jackson akizungumza mbele ya mamati ya sheria katika seneti mjini Washington, March 23, 2022.
Jaji Ketanji Brown Jackson akizungumza mbele ya mamati ya sheria katika seneti mjini Washington, March 23, 2022.

Mteule wa Rais wa Marekani Joe Biden katika mahakama ya juu Marekani, Jaji Ketanji Brown Jackson siku ya Jumatano kwa mara nyingine alitetea rekodi yake kwa wajumbe wa Republican wa kamati ya sheria katika seneti katika siku yake ya tatu ya mahojiano ili apate kuthibitishwa.

Mahojiano ya Jumatano yanafuatia kikao cha Jumanne ambacho kiliendelea hadi jioni. Wakat wa kipindi hicho cha maswali na majibu, wa-Democrat walitumia muda wao mwingi waliopewa kuzungumza kwa moyo mkunjufu na Jackson, badala ya kuuliza maswali zaidi.

Wa-Republican kwa upande mwingine walimhoji mwanamke huyo wa kwanza mweusi kuwahi kuteuliwa katika mahakama ya juu zaidi Marekani, wakiangazia kile wanachoamini ni rekodi yake ya msimamo wa wastani, na kueleza kwamba Jaji Jackson ni mpole kwenye sula la uhalifu.

Wafuasi wa Republican walirejea haraka kwenye mada hiyo siku ya Jumatano huku seneta M-republican Thom Tillis akieleza Jackson alikuwa na tabia ya upole ambayo ilimfanya awe mpole sana katika kutoa hukumu kama jaji wa serikali kuu. Jaji Jackson alitoa jibu kwa upana akisema mara nyingi alitaka kuwaeleza washtakiwa athari za vitendo vyao kwa lengo la kupunguza uwezekano kwamba wangefanya uhalifu zaidi watakapoachiliwa.

XS
SM
MD
LG