Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:01

Belarus yaiomba Russia kuisaidia kuimarisha ulinzi wake


Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko walipokutana huko Moscow, Apr. 6, 2023. (Gavriil Grigorov, Sputnik, Kremlin Pool Photo via AP)
Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Belarus Alexander Lukashenko walipokutana huko Moscow, Apr. 6, 2023. (Gavriil Grigorov, Sputnik, Kremlin Pool Photo via AP)

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko alisema Jumatatu nchi yake inahitaji kuhakikishiwa ulinzi na Russia, kulingana na kituo cha matangazo cha serikali BelTA.

Maoni yamekuja wakati Lukashenko akiwa mwenyeji wa Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu.

Kulingana na BelTA, Lukashenko alieleza mazungumzo yake na Rais wa Russia Vladimir Putin wiki iliyopita, na kusema viongozi hao wawili walijadili umuhimu wa Russia kuilinda Belarus “ kama eneo lake binafsi” iwapo kutakuwa na uchokozi unaoelekezwa Belarus.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Putin alielemewa na ukosoaji mwezi uliopita alipotangaza kuwa Russia itapeleka silaha za nyuklia za mbinu ya hali ya juu huko Belarus.

Majeshi ya Russia pia yameitumia Belarus kama ni eneo la kuanzisha uvamizi kamili huko Ukraine zaidi ya mwaka moja uliopita, baada ya washirika wawili kusisitiza walikuwa wanafanya mazoezi ya kijeshi tu na hawakuwa na mpango wa kuishambulia Ukraine.

Mikoa miwili ya Ukraine – Kharkiv upande wa kaskazini mashariki na Zaporizhzhia huko kusini mashariki – zimeshambuliwa na makombora, roketi na mizinga ya Russia wakati wa wikiendi, jeshi la Ukraine limeripoti Jumapili.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari yahe Associated Press, Agence France-Presse na Reuters.

XS
SM
MD
LG