Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 17:17
VOA Direct Packages

Putin na afisa wake wasakwa na ICC kwa madai ya kuteka watoto wa Ukraine


Rais wa Russia, Vladimir Putin.
Rais wa Russia, Vladimir Putin.

Afisa wa Russia ambaye ameshitakiwa pamoja na rais wa taifa hilo Vladimir Putin na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa madai ya kuwateka nyara maelfu ya watoto wa Ukraine, amesema Jumatano kwamba Moscow ipo tayari kutoa ushirikiano kwa minajili ya watoto hao.

Maria Lvova Belova ambaye ni kamishna wa watoto kwenye ofisi ya rais amesema kwamba “ kwa bahati mbaya hakuna mawasiliano rasmi kupitia mitandao rasmi na Ukraine, ingawa tupo tayari kushirikiana na wahusika wote.” Ameongeza kusema kwamba kufikia sasa hawajapata mwaliko rasmi kando na kupitia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Lvova Belova amezungumza kwa njia ya video kwa vile hawezi kusafiri kimataifa kwa hofu ya kukamatwa na kupelekwa kwenye mahakama ya ICC mjini the Hague. Tayari hati ya kukamatwa pamoja na Putin ilitolewa na ICC hapo Machi 17.

XS
SM
MD
LG