Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 09:44

Russia yashindwa kuharibu mfumo wa nishati wa Ukraine


Kampeni ya Russia ya kuharibu vibaya mfumo wa nishati wa Ukraine msimu huu wa baridi huenda imeshindwa, wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema katika ujumbe wa Twitter Jumamosi.

Wakati mashambulizi makubwa ya Russia dhidi ya nishati ya Ukraine yamepungua tangu mapema Machi, kulingana na wizara hiyo, Russia imeendelea na mashambulizi madogo ambayo hayajaleta athari kubwa katika mpango wake wa kuathiri usambazaji wa nishati wa Ukraine.

Watoto 31, waliotekwa na Russia kutoka mikoa ya Kherson na Kharkiv wamerejea Ukraine baada ya kutenganishwa na wazazi wao kwa miezi kadhaa, kulingana na shirika la hisani la Save Ukraine.

Kutenganishwa kwa watoto wa Ukraine na familia zao kumesababisha mashtaka ya uhalifu wa kivita kufunguliwa dhidi ya Rais wa Russia Vladimir Putin.

Wakati huohuo afisa mkuu wa wizara ya fedha ya Marekani, Ijumaa alisema hakuna ushahidi wa kuonyesha China inatoa msaada wa vifaa kwa Russia, licha ya kuonekana uwepo wa urafiki wa Beijing na Kremlin.

XS
SM
MD
LG