Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 17:50

Mshindi wa Tuzo ya Nobeli ya Amani Ales Bialiatski ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela


Ales Bialiatski, kiongozi wa kundi la kutetea haki za binadamu cha Belarus, Vyasna, akikaa nafasi ya washtakiwa wakati wa kesi yake mjini Minsk, Januari 5, 2023..

Mshindi wa Tuzo ya Nobeli ya Amani Ales Bialiatski amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na mahakama moja huko Belarus.

Bialiatski ni muanzilishi wa kikundi maarufu cha haki za binadamu cha Viasna, huko Belarus ambacho kimekuwa kikitoa msaada wa kisheria na kifedha kwa waandamanaji, kufuatia wimbi la ghasia la mwaka 2020.

Ghasia hizo zilitokea baada ya mzozo wa matokeo ya uchaguzi uliomrejesha tena madarakani Rais Alexander Lukashenko, wadhifa anaoushikilia kwa zaidi ya miaka 30.

Lukashenko, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais wa Russia Vladimir Putin, aghlabu anajulikana kama “dikteta wa mwisho” barani Ulaya.

Bialiatski amesema kuwa anashtakiwa kwa sababu za kisiasa.

Bialiatski ni miongoni mwa watu watatu waliopokea mwaka jana Tuzo ya Nobeli ya Amani, pamoja na vikundi vya haki za binadamu vya Russia na Ukraine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG