Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 00:37

Ukraine inajiandaa kwa mashambulizi makubwa ya Russia mwezi huu


Waziri wa ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov

Ukraine Jumapili imesema imejiandaa kwa uwezekano wa mashambulizi makubwa ya Russia mwezi huu ambayo yatakuwa sambamba na kumbukumbu ya uvamizi wa Russia Februari 24, lakini inasema ina uwezo wa kukabiliana na vikosi vya Russia.

Waziri wa ulinzi Oleksii Reznikov ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba Russia inaweza kufanya shambulizi kwa sababu za “kiishara” ingawa vikosi vya Moscow havijajiandaa kijeshi.

“Licha ya mambo yote, tunatarajia uwezekano wa mashambulizi ya Russia mwezi huu wa Februari,” Reznikov amesema.

Reznikov amesema mashambulizi ya Russia yanaweza kuanzishwa mashariki mwa nchi ambako mapigano yamekuwa yakifanyika kwa miezi kadhaa na Russia inajaribu kuuteka mkoa wote wenye viwanda vingi wa Donbas, au pengine kusini mwa nchi, ambako inataka kupanua njia yake ya ardhini kuelekea Peninsula inayoikalia kimbavu ya Crimea iliyonyakua kinyume cha sheria mwaka 2014.

Waziri huyo wa ulinzi amekadiria kuwa wanajeshi 12,000 wamepiga kambi kwenye kambi za kijeshi huko Belarus, lakini idadi hiyo ni ndogo kuanzisha shambulizi kubwa kaskazini mwa Ukraine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG