Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 20, 2021 Local time: 07:10

Baraza la Wawakilishi kupiga kura kudhibiti uwezo wa Trump kuanzisha vita


Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani

Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani litapiga kura hii leo kupitisha azimio litakalozuia uwezo wa Rais Donald Trump kuanzisha vita na Iran.

Spika wa baraza hilo linalodhibitiwa na Wademokrats Nancy Pelosi anasema wanachukuwa hatua hiyo kwa sababu uamuzi wa Rais Trump kuruhusu ndege isiyo na rubani kumshambulia na kumuua afisa wa juu wa Iran Jenerali Qasem Solemani wiki iliyopita ulifanyika bila ya kulishirikisha bunge.

Azimo hilo linatarajiwa kuidhinishwa kwa urahisi na baraza la wawakilishi lakini itakuwa vigumu kukubaliwa katika baraza la Seneti linalodhibitiwa na Warepublican.

Wakati huo huo wabunge wengi hawajaridhika na maelezo ya maafisa wa White House juu ya sababu walizotoa, jana kuhusu kwa nini Trump alichukua uamuzi huo.

Seneta Mrepublican Mike Lee ni moja wapo wa wabunge walohudhuria kikao maalum pamoja na maafisa wa white house.

Mike Lee Seneta Mrepublican amesema : "Si jambo linalokubalika kwa maafisakutoka utawala, sijali ikiwa ni kutoka CIA, au wizara ya ulinzi au kwengineko kuja na kutuambia hatuwezi kujadili na kuzungumzia umuhimu wa hatua ya kijeshi dhidi ya Iran. Hiyo haiambatani na maadili ya kimarekani. Inakwenda kinyume cha katika na ni makosa."

Hii leo vile vile baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana kujadili mvurtano kati ya Marekani na Iran, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea huko Mashariki ya Kati na Umoja wa Ulaya ili kutafuta suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huu.

Kwa upande waka Papa Francis akitoa hotuba yake ya kila mwaka juu ya hali ya dunia amezihimiza Marekani na Iran kuepusha uwezekano wa kutokea vita vikubwa huko Mashariki ya Kati na kufuata njia ya majadiliano.

Papa Fransis amesema : "Kwa hivyo kwa mara nyingine ninatoa wito kwa pande zote zinazohusika kuepusha kuzidisha ugomvi na kuendelea na juhudi zamazunguzo, kustahmiliana na kuheshimu sheria za kimataifda.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG