Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:35

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani mauwaji ya mwandishi wa Al Jazeera


Polisi wa Israel wana wavamia familia na marafiki wa mwandishi habari Shireen Abu Akleh walipokua wanakwenda kumzika
Polisi wa Israel wana wavamia familia na marafiki wa mwandishi habari Shireen Abu Akleh walipokua wanakwenda kumzika

Serikali ya Palestina imesema Jumamosi kwamba, itakaribisha msaada wa kimataifa kufanya uchunguzi kuhusiana na mauwaji ya mwanadishi habari mashuhuri wa Al Jazeera.

Serikali ya Israel nayo inasema itafanya uchunguzi kuhusu kuzuka ghasia wakati wa maziko yake, ili kufahamu kilichotokea.

Polisi wa Israel walivamia umati wa watu walokua wanabeba jeneza la mwandishi habari mkongwe Shireen Abu Akleh, kupitia mji wa kale wa Jerusalem kwenda kumzika jana Ijuma, kitendo kilicho laaniwa na Jumuia ya Kimataifa.

Ghasia hizo zimezidisha hasira kutokana na mauwaji ya Abu Akleh ambayo yanatishia kuongeza mvutano ambao umezuka tangu mwezi wa March.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel Omer Barlev, amesema kwamba pamoja na mkuu wa polisi, wameteua jopo la kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kilichotokea wakati wa maziko.

Maafisa wa Palestina wameeleza kifo cha Abu Akleh, aliyekua anaripoti uvamizi wa Israel kwenye kambi ya wakimbizi katika mji wa Jenin, Ukingo wa Magharibi, kuwa mauwaji yaliyofanywa na wanajeshi wa Israel.

Awali, Isreal ilisema huwenda alishambuliwa na wapiganaji wa Palestina, lakini tangu wakati huo maafisa wamebadili msemo wao, wakisema kuna uwezekano aliuliwa kutokana na risasi kutoka wanajeshi wake.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa kwenye kikao maalum limelaani vikali mauwaji hayo na kutoa wito wa kufanyika mara moja uchunguzi wa kina ulowazi na usiopendelea upande wowote.

XS
SM
MD
LG