Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:39

Waombolezaji wajitokeza Jerusalem kumzika Mwandishi Shireen Abu Akleh


Wapalestina wakiomboleza kifo cha mwandishi Shireen Abu Akleh. REUTERS/Raneen Sawafta
Wapalestina wakiomboleza kifo cha mwandishi Shireen Abu Akleh. REUTERS/Raneen Sawafta

Maelfu ya Wapalestina na Waisraeli wamehudhuria Ijumaa maziko ya mwandishi wa habari mashuhuri na mahiri wa shirika la televisheni la Al-Jazeera Shireen Abu Akleh.

Maziko yake yamefanyika katika mji wa kale wa Jerusalem ambao umekuwa katika hali ya juu kabisa ya usalama.

Waisraeli na Wapalestina wanalaumiana juu ya nani aliyemua mwandishi habari huyo Mmarekani mwenye asili ya Palestina mapema wiki hii alipokua anaripoti uvamizi wa jeshi la Israel kwenye kambi kuu ya Jenin.

Israel imeelezea masikitiko yake kwa kifo chake na kutoa wito wa uchunguzi wa pamoja ambao wapalestina wanakataa.

Mwili wa Abu Akleh aliyekuwa na umri wa miaka 51 ulisafirishwa kutoka ukingo wa Magharibi hadi Jerusalem Mashariki na ibada ya maziko ilifanyika kwenye kanisa kuu la mji wa kale jeneza lake limebebwa na maelfu ya watu hadi kaburini.

Wapalestina wa Jerusalem wamefunga biashara zao ili kutoa heshima zao kwa Abu Akleh.


Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari

XS
SM
MD
LG