Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 16:37

Baraza la Seneti lapitisha mswaada wa kuimarisha huduma za afya kwa wanajeshi wastaafu


US Capitol dome at night - Congress - Washington

Baraza la Senati la Marekani limepitisha mswaada wa kuimarisha huduma ya afya na malipo kwa mamilioni ya wanajeshi wastaafu.

Mswaada huo unatilia maanani wanajeshi wastaafu wenye ulemavu, na waliopata majeraha mabaya wakati walipokuwa kazini nchini Iraq na Afghanistan.

Mswaada huo sasa unasubiri Saini ya Rais Joe Biden na kuwa sheria. Biden amesema kwamba wanajeshi hao wa zamani wanahitaji huduma bora ya afya.

Baraza la Senati lilikuwa limepitisha mswaada huo kwa kura nyingi lakini mchakato ulikwama wiki iliyopita baada ya warepublica kujaribu kubadilisha baadhi ya vipengele kwenye mswaada.

Hatua ya warepublican iliyakasirisha makundi ya kutetea haki za wanajeshi wa zamani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG