Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:09

Seneta Marekani anahoji msaada kwa Rwanda


Mwenyekiti wa Kamati ya Uhusiano ya  Nje katika baraza la Seneti  la  Marekan akiwa mjini Washington, DC
Mwenyekiti wa Kamati ya Uhusiano ya  Nje katika baraza la Seneti  la  Marekan akiwa mjini Washington, DC

Mwenyekiti wa Kamati ya Uhusiano ya  Nje katika baraza la Seneti  la  Marekani alisema atasimamisha msaada wa usalama wa Marekani kwa Rwanda katika Bunge  kutokana na wasiwasi kuhusu rekodi ya haki za binadamu ya serikali ya Rwanda na jukumu lake katika mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Katika barua kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, Seneta Robert Menendez alitoa wito wa tathmini ya kina ya sera ya Marekani kwa Rwanda.

Menendez alisema ataanza kwa kusimamisha dola milioni kadhaa kuwasaidia walinda amani wa Rwanda wanaoshiriki katika shughuli za Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa barua hiyo, ambayo ilivujishwa kwenye vyombo vya habari na ambayo ofisi yake ilithibitisha kuwa ni ya kweli. Hatua hiyo iliyochukuliwa ni utaratibu wa Seneti unaozuia hoja kufika kwenye ngazi ya kupiga kura.

Menendez alisema anahofia kwamba uungaji mkono wa Marekani kwa jeshi la Rwanda wakati linatumwa Congo na kuwaunga mkono waasi utatoa ishara ya kutatanisha kwamba Marekani inaidhinisha kimya kimya vitendo hivyo.

XS
SM
MD
LG