Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 09:03

Baraza Kuu la Libya lapiga kura kubadilisha kiongozi wake


PICHA YA MAKTABA: Waziri Makuu wa Libya Abdulhamid al-Dbeibah.
PICHA YA MAKTABA: Waziri Makuu wa Libya Abdulhamid al-Dbeibah.

Baraza kuu la taifa la mashauriano nchini Libya (HSC) lilibadilisha kiongozi wake katika kura iliyopeperushwa kwenye televisheni siku ya Jumapili, na kuongeza hali ya sintofahamu katika mzozo wa kisiasa kuhusu udhibiti wa serikali na njia ya kuelekea uchaguzi.

HSC yenye makao yake makuu mjini Tripoli ina usemi katika masuala makubwa ya kisiasa chini ya masharti ya makubaliano ya kisiasa ya mwaka 2015 na imekuwa ikifanya mazungumzo na bunge kuu la Libya, Baraza la Wawakilishi, ambalo lina makao yake makuu mashariki mwa nchi hiyo.

Wanachama wa baraza hilo walimchagua Mohammed Takala katika duru ya pili ya kura, kwa kura 67 dhidi ya 62, na kumuondoa Khaled al-Meshri ambaye ameongoza baraza hilo lenye makao yake mjini Tripoli tangu 2018. Meshri alimpongeza Takala kwa ushindi wake.

HSC na bunge wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia ya uchaguzi chini ya shinikizo la Umoja wa Mataifa, lakini wote wamekuwa na azma ya kubadilisha serikali ya mpito ya Tripoli kabla ya kura yoyote ya kitaifa.

Waziri Mkuu Abdulhamid al-Dbeibah, anayeonekana kuwa mpinzani wa kisiasa wa Meshri na spika wa Bunge Aguila Saleh, amesema hatajiuzulu hadi baada ya uchaguzi, na mwaka jana alipambana na juhudi za muda mfupi za kumwondoa madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG