Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:24

Shirika la kutetea haki za binadamu latoa wito wa msaada kwa wahamiaji 360 waliokolewa na maafisa wa Libya


Wahamiaji kutoka nchi za Afrika za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wanadai kuachwa jangwani na maafisa wa Tunisia bila maji, wakikaa chini katika eneo lisilokaliwa na watu karibu na mji wa mpakani wa Libya wa Al-Assah, Julai 16, 2023.

Kundi la kiarabu la kutetea haki Jumatatu limetoa wito wa msaada wa kimataifa kwa wahamiaji 360 kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao waliokolewa na maafisa wa Libya baada ya kuachwa jangwani na polisi wa Tunisia kwenye mpaka na Libya.

Shirika hilo la haki za binadamu lenye makao yake mjini Cairo (AOHR) limepongeza hatua ya Libya kuwapokea wahamiaji hao “waliopitia hali ngumu ya kibinadamu” kabla ya kuchukuliwa na walinzi wa mpakani wa Libya.

“Kulingana na walinzi wa mpakani wa Libya, wahamiaji 360 wakiwemo wanawake na watoto wanahitaji msaada wa haraka na matibabu, tawi la AOHR nchini Libya limesema, likiwasihi maafisa wa Libya “kuliruhusu shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi na shirika la kimataifa la uhamiaji (IOM), kukutana na wahamiaji hao na kuwasaidia kwa taratibu za kisheria”.

IOM nchini Libya Jumatatu ilisema itatoa msaada wa dharura wa kibinadamu kwa wahamiaji waliookolewa kwenye mpaka na Tunisia.

Forum

XS
SM
MD
LG