Kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Misri mapema mwezi Julai kunaongeza matumaini ya kumaliza mizozo huko Mashariki ya Kati na Afrika.
Uturuki na Misri zote zilihusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ethiopia na Libya na wachambuzi wanatumai kurejeshwa kwa hivi karibuni kwa uhusiano kamili wa kidiplomasia kati ya Cairo na Ankara kutasaidia kupunguza mivutano katika kote Mashariki ya Kati na Afrika.
Inaweza kuiathiri Misri, walau suala ambalo walilonalo nchini Ethiopia kwa sababu nchi zote mbili zinaunga mkono pande tofauti za mzozo. Kwa hivyo kwa ujumla nadhani hili ni jambo jema. Nadhani ni msaada kwa Libya pia kwa sababu pande zote mbili zinaunga mkono vikundi tofauti nchini Libya. Nadhani mkwamo huu umeendelea kwa muda mrefu sana. Ni wakati kwa mamlaka zilizopo kutafuta njia ambayo kila mtu anaweza kukubaliana nalo.
Uingialiaji kijesjhi wa Uturuki katika kuiunga mkono Serikali ya Makubaliano ya Umoja wa Kitaifa ya Libya dhidi ya vikosi vinavyoungwa mkono na Misri vya Jenerali Khalifa Haftar ulipelekea Uturuki na Misri kukaribia katika hali ya mapambano ya moja kwa moja. Sasa Ankara inasema ushirikiano wa kiuchumi unatoa njia ya kusonga mbele.
Lakini kuwepo kwa jeshi la Uturuki nchini Libya bado ni kikwazo huku Cairo ikitaka liondolewe.
Utajiri mkubwa wa nishati nchini Libya unatoa msukumo mkubwa wa ushirikiano kati ya Uturuki na Misri.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametia saini mkataba wa mabilioni ya dola na Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia wote wakiwa washirika wa Misri. Wachambuzi wanasema mikataba kama hiyo itasaidia kuhakikisha mustakabali wa ukaribu mpya wa Uturuki na Misri, pamoja na hayo pia kuondolewa kwa jeshi linalovuruga eneo hilo.
Forum