Marekani ni mwenyeji wa Mkutano wa kundi la mawasiliano la Ukraine ili kutafuta silaha zaidi na risasi kwa ajili ya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.
Wanachama wa NATO na nchi washirika watasubiri kusikia ni aina gani ya vifaa vya kijeshi Kyiv inahitaji.
Kufuatia Mkutano huo wanachama 31 na ukraine watashiriki katika sehemu ya kwanza ya baraza la NATO kuhusu ukraine katika kiwango hicho.
Baraza hilo liliundwa rasmi mwezi Julai kwa ajili ya kuileta karibu Kyiv na washirika.
Inaruhusu NATO na Kyiv kujadiliana masuala yenye ushawishi wa pamoja na wasiwasi uliopo.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aliwaambia waandishi wa habari waliosafiri naye kwenda Brussels kwamba washirika kadhaa watatangaza kwamba wanatuma silaha zaidi na misaada mingine Kyiv ambapo mahitaji muhimu ni mifumo zaidi ya ulinzi wa anga na silaha.
Forum