Mkutano huo ni wa kwanza wa Zelensky, nchini Romania, tangu uvamizi wa Russia, Februari mwaka jana.
Romania, mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO, imekuwa ikiunga mkono juhudi za vita vya Ukraine, huku rais Iohannis akisema kuwa nchi yake inalenga kuisaidia Ukraine, kushinda vita.
Zelenskyy, alisisitiza uhusiano thabiti wa mataifa hayo mawili na kuishukuru Romania, kwa kuendelea kuiunga mkono kijeshi na kibinadamu.
Zelenskyy amesema kwenye mtandao wa X, kwamba uhusiano wa nchi hizo mbili ni muhimu kwa utulivu kwa Ulaya na kwingineko.
Forum