Polisi wa kupambana na ghasia huko Ubelgiji wametumia mabomba ya maji kuwatawanya wanaharakari wa itikadi kali za mrengo wa kulia wanaopinga wahamiaji walopambana na waombolezi.
Waandamanaji wa mrengo wa kulia washambulia waombolezi Brussels

1
Jumapili ya Pasaka ilianza kwa amani pale mamia ya watu walipojitokeza na kutoa heshima zao kwa waathiriwa wa mabomu ya kigaidi ya Brussels, Ubelgiji, March 27, 2016. (H. Murdock/VOA)

2
Mnamo wiki nzima uwanja mbele ya jengo la soko la hisa la Ubelgiji umegeuka kua eneo la makumbusho ya waathiriwa wa mabomu ya Brussels na kutolewa ujumbe wa umoja. Na bango linalosema sio kwa jina la Uislamu. (H.Murdock/VOA)

3
Wanaharakati wa mrengo wa kulia walipojitokeza waombolezi wakawazomea na kuwaeleza kua ni mafashisti. (H. Murdock/VOA)

4
Polisi wa usalama waliongezwa mara moja katika eneo la makumbusho ambalo tayari lilikua linalindwa vikali siku ya Pasaka wakati wanaharakati wa mrengo mkali wa kulia kujitokeza na kupiga makelele wakitumia makauli kulaani uislamu mjini Brussels. (H. Murdock/VOA)