Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:10

Mahakama ya Rufaa Yatupilia Mbali Amri ya Rais Trump Kuhusu Wahamiaji


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Amri ya kiutendaji ya Rais Trump imezuiliwa isitumike na Mahakama ya Rufani nchini Marekani.

Mahakama hiyo imesema haitozuia maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya chini ambayo ilitupilia mbali amri ya kiutendaji ya rais.

Rais Trump alitoa amri ya muda kuzuia watu kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani kwa madai ya vitisho vya kigaidi ambavyo alisema vinahatarisha usalama wa taifa.

Mara baada ya mahakama ya rufaa kutoa uamuzi Rais ametuma ujumbe wa Twitter akisema: " Tutaonana mahakamani, usalama wa taifa letu uko matatani."

Uamuzi huu umefanywa na jopo la Majaji watatu kutoka katika mahakama ya rufaa jijini San Francisco na kwa pamoja wamekataa kuzuia amri ya Mahakama ya chini iliyokataza amri hiyo ya Trump.

“Tunaamini kwamba serikali haijaonyesha kwamba inahoja ya kufanya rufaa yao iwe na mashiko, pia haijaonyesha kuwa amri ya kuwazuia wahamiaji ikiondolewa italeta madhara yasiokadirika nchini Marekani, tamko lilitolewa na Mahakama ya rufaa limesema.

XS
SM
MD
LG