Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 14:23

Suala la Uhamiaji Marekani laelekea Mahakama ya Rufaa


Jayne Novak, kushoto, akiwa katika furaha na mumewe Allen Novak na mtoto wao Nikta mara baada ya kuwasili kutoka Iran
Jayne Novak, kushoto, akiwa katika furaha na mumewe Allen Novak na mtoto wao Nikta mara baada ya kuwasili kutoka Iran

Mahakama ya Rufaa ya Marekani inatarajiwa kusikiliza hoja Jumanne katika ushindani wa kisheria kuhusu amri ya kiutendaji ya Rais Donald Trump.

Amri itayopiganiwa mahakamani ni ile iliyozuia mpango wa kuingiza wakimbizi nchini na kuwakataza watu kutoka mataifa saba yenye waislamu wengi kuingia Marekani.

Muhtasari wa hoja iliyowasilishwa na Wizara ya Sheria inaitetea amri hiyo na kusema “ni zoezi la kisheria lilioko ndani ya mamlaka ya rais katika kuwaingiza wahamiaji Marekani na kuwapokea wakimbizi.

Inasema agizo la jaji wa mahakama ya rufaa la kusitisha amri ya kuwazuia wahamiaji na wakimbizi ni kosa na liko nje ya madai ya kisheria ya Jimbo hilo.

Majimbo 15 yafungua kesi

Katika kesi hii majimbo ya Washington na Minnesota ndio wadai. Tayari wanasheria wakuu wa majimbo 15, umoja wa haki za wananchi Marekani, na kikundi cha makampuni takriban 100 wameshaungana nao katika kesi hiyo.

Wakati pia baadhi ya makampuni yamewasilisha muhtasari wa madai wakikubaliana na amri ya kuzuiwa wahamiaji na wakimbizi.

Mawaziri wastaafu wa mambo ya nje, John Kerry na Madeleine Albright wanasema amri ya kiutendaji ilikuwa “imetayarishwa vibaya, imetekelezwa ovyo na haikuelezewa vizuri.”

Amri Inahatarisha Usalama wa Taifa

“Tunaona amri hii kama kwamba mwisho wa yote itahatarisha usalama wa taifa la Marekani kuliko kulifanya liwe na amani," wamesema, kinyume na maelezo ya Trump kwamba amri ya kukataza wahamiaji itaimarisha usalama wa taifa. Hata hivyo kesi hii inaelekea kuwa itaishia kwenye Mahakama Kuu ya Marekani.

Mchambuzi mmoja ambaye ni wakili huko New York, Dan McLaughlin, ameiambia VOA kuwa mahakama ya juu ya Marekani ina historia ya kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuhimili upande wa Trump iwapo kesi itafika katika mahakama hiyo.

Bunge la Marekani lina maamuzi

Mahakama kuu imekuwa ikikubali kwa muda mrefu kwamba Bunge lina maamuzi ni kama vile yasiyo na kikomo katika kuamua nani anaweza kuingia nchini, maamuzi ambayo yanawapa haki kukataa watu kutoka nchi fulani fulani, kama ilivyokuwa imefanya wakati wa kadhia ya wahamiaji wa Kichina mwaka 1880,” amesema McLaughlin, ambaye pia anaandika makala katika tovuti ya habari ya waconservative.

“Kwa kuwa rais anategemea mamlaka aliyopewa na Bunge, ana amri pana kufanya maamuzi ndani ya sheria, hata kama unafikiria sera zake ni sawa au vinginevyo.”

Lakini McLaughlin amesema pia kuwa kampeni ya Trump wakati wa uchaguzi juu ya kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu inaweza kuja kumharibia katika kesi hii huko Mahakama Kuu.

Hakuna shaka kwamba rais ana maoni yaliyotangulia ambayo yatafanya kesi hiyo kuwa ngumu zaidi kwake kuitetea (amri yake ya kiutendaji ya uhamiaji) katika mahakama na umma,” amesema.

XS
SM
MD
LG