Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 13:27

Amri ya Kiutendaji ya Rais Trump Huenda Ikaishia Mahakama Kuu


Rais wa Marekani, Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump

Watalaamu wa sheria karibu wote wanakubaliana kwamba kikatiba amri ya kiutendaji ya rais Donald trump itaishia katika mahakama kuu ya Marekani.

Amri hiyo inapiga marufuku kwa muda kwa watu kuingia nchini marekani kutoka mataifa saba yenye waislamu wengi na wakimbizi.

Kesi kadhaa zinazohusu marufuku ya kusafiri hivi sasa zinafanyiwa kazi na zinaelekea kufikishwa katika mahakama mbali mbali humu nchini, moja tayari inaonekana inatarajiwa kuishia katika mahakama ya juu zaidi hapa nchini.

Mfumo wa Mahakama

Mfumo wa mahakama nchini marekani ni kama pyramid. Unaanzia chini ambako kuna mahakama takriban 94 ambazo zinaitwa ni mahakama za wilaya. Kama mtu mmoja au taasisi inataka kumwajibisha mwingine huko ndiyo kwa kuanzia.

Katikati kuna mahakama 13 za rufaa. Kama upande mmoja au mwingine haukubaliani na uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini, basi wanaendelea na kesi yao katika mahakama za rufaa.

Juu kabisa kuna mahakama kuu, hii ikiwa ni mahakama ya juu ya rufaa. Itakachoamua mahakama hii ya juu basi kitakubalika.

Mahakama ya Wilaya

Tukiangalia mahakama za wilaya kila jimbo lina mahakama hizo pamoja na jiji kuu la marekani district of Columbia. Mahakama hizi zinasuluhisha mizozo kwa kuangalia ukweli na kutumia misingi ya kisheria kuamua nani yuko sahihi.

Kesi kadhaa zinaweza kuwasilishwa dhidi ya marufuku ya kusafiri katika mahakama za wilaya. Taasisi ya civil rights litigation clearing house imerekodi 60 kati ya hizo, baadhi ya 20 tayari zimetupiliwa mbali. Nyingi ya kesi hizo zilifikishwa kwa niaba ya watu binafsi au makundi ya watu ambao hawakuruhusiwa kuingia marekani kutokana na amri ya kiutendaji.

Wanadai kuwa haki zao za msingi zimekiukwa na utaratibu unaohusika kwa mujibu wa sheria haukufuatwa, pia wanadai kwamba katiba inawapa dhamana ya uhuru wa dini ambao umtenguliwa kwasababu wao ni waislamu kwa kujumuishwa katika amri hiyo.

Kufikishwa Kesi katika Majimbo

Kesi katika mahakama za wilaya zilifikishwa katika majimbo mbali mbali. Januari 29, siku mbili baada ya kutiwa saini amri hiyo, jaji wa mahakama ya new York alizuia kwa muda wa wiki moja kwa watu kuondolewa nchini. Februari sita jaji katika jimbo la Washington aliizuia amri nzima ya kiutendaji na kuruhusu wakimbizi wote na watu kutoka mataifa saba yaliyowekewa marufuku kuanza kusafiri kuja nchini marekani.

Jukumu la mahakama ya rufaa ni kuangalia iwapo sheria ilitumika kwa usahihi katika mahakama za chini. Mahakama za rufaa zinakuwa na majaji watatu na hakuna jopo la wataalamu wa kusikiliza kesi hizo. Wanasheria wa wizara ya sheria wanadai kwamba rais ana mamlaka mapana ya kuangalia nani anaingia nchini na kwamba kwa kiasi kikubwa ana kinga kutokana udhibiti wa mahakama. Trump anasema amri ni muhimu kuwalinda wamarekani dhid ya magaidi.

Majimbo ya Washington na Minnesota yanasema marufuku inaumiza maslahi ya kuchumi na itasababisha vurugu.

Jumapili mahakama ya rufaa ilikataa haraka kufuta maamuzi wakati ikisubiri kutathimi kesi hiyo. Iliweka jana jumatatu mchana kwa kuwasilisha malalamiko zaidi.

Wanadiplomasia na Maafisa wa Usalama

Wanadiplomasia wa juu wa zamani na maafisa usalama wa taifa, na takriban makampuni 100 ya kiufundi, maprofesa a sheria 280 na idadi ya taasisi kadhaa za kisheria zimewasilisha malalamiko mahakamani.

Bila ya kujali upande gani unashinda katika ngazi ya mahakama ya rufaa, aliyeshindwa huenda akaichukua kesi hiyo kwenye mahakama ya juu kabisa.

Kwa kawaida majaji tisa wa mahakama kuu hawachukui kesi zote ambazo zinakatiwa rufaa kwao. Wanachagua ingawaje majaji huenda wakaichukua kesi hii ya marufuku ya kusafiri.

Baada ya kifo cha jaji Antonin scalie februari mwaka jana, mahakama hivi sasa ina upungufu wa jaji mmoja. Hii inaonyesha wanaweza kufungana katika maamuzi. Kama mahakama itashindwa kupata wingi wa majaji watano dhidi ya watatu kesi hiyo itarejea uamuzi wa mahakama ya rufaa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Khadija Riyami

XS
SM
MD
LG