Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:02

Amnesty International yatoa tamko kuhusu kifo cha Msando wa IEBC


Mwenyekiti wa Tume Huru inayosimamia uchaguzi na Mipaka Kenya, Wafula Chebukati akizungumza na waandishi baada ya vikundi vya kijamii kuandamana kulaani mauaji ya Chris Msando,
Mwenyekiti wa Tume Huru inayosimamia uchaguzi na Mipaka Kenya, Wafula Chebukati akizungumza na waandishi baada ya vikundi vya kijamii kuandamana kulaani mauaji ya Chris Msando,

Mauaji ya Chris Msando na matukio mengine kabla ya uchaguzi Agosti 8 umepelekea wingu la wasiwasi mkubwa nchini Kenya, Shirika la Haki za Binadamu (Amnesty International) limesema.

Shirika hilo lenye kufuatilia haki za raia Jumatano limeitaka serikali kushughulikia mauaji ya afisa huyo wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kikamilifu na mambo mengine- zikiwemo kauli za viongozi na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali.

Msando inaaminika kuwa aliuawa mapema Jumamosi asubuhi na mwili wake kutelekezwa katika kichaka eneo la Kikuyu, Kaunti ya Kiambu.

Mwili wake ulitambuliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Jumatatu asubuhi.

“Mauaji haya ya kinyama yamewashitua Wakenya wengi na kuongeza wasiwasi wa kuwepo uvunjifu wa amani,” amesema Muthoni Wanyeki, Mkurugenzi wa Amnesty International katika eneo la Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu.

Mkurugenzi huyu ameeleza kuuliwa kwa Msando kama ni kitendo kiovu kuliko vyote katika wakati wa uchaguzi mwaka huu lakini amesema hili sio pekee linaloweza kuwa na msukumo wa kupandikiza wasiwasi katika jamii.

“Serikali ni lazima ichukue hatua thabiti kuleta utulivu kutokana na hali kuwa tete na kuwahakikishia wapiga kura usalama wao ni kipaumbele chao,” amesema.

XS
SM
MD
LG