Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 13:16

Almasi kubwa nadra kupatikana yagunduliwa Angola


Almasi ya karate 170 ilipatikana kutoka Lulo, Angola iliyochimbwa na Kampuni ya Lucapa Diamond July 27, 2022.
Almasi ya karate 170 ilipatikana kutoka Lulo, Angola iliyochimbwa na Kampuni ya Lucapa Diamond July 27, 2022.

Wachimba madini wa kaskazini mashariki mwa Angola wamegundua jiwe la almasi adimu, rangi ya  waridi wanaloamini kuwa ni kubwa zaidi ya aina yake kupatikana tangu miaka 300 iliyopita.

Katika eneo la wachimbaji wa Australia nchini angola, wameitaja almasi ya karati 170 Lulo Rose.

Wamesema almasi hiyo itauzwa katika mashirika ya kimataifa na kampuni ya masoko ya almasi ya Angola.

Upatikanaji huo umekaribishwa na serikali ya Angola. “Rekodi hii ya almasi ya waridi iliyopatikana katika Lulo inazidi kuonyesha Angola kama nchi muhimu duniani katika machimbo ya almasi.”

Waziri wa madini Diamantino Azevedo amenukuliwa akisema katika taarifa kwamba jiwe kama hilo limewahi kuuzwa kwa bei ya kubwa sana.

Lilikuwa jiwe la rangi ya waridi lenye karati 59 liliuzwa kwa dola milioni 71.2 mwaka 2017 ikiwa ni bei ya juu kuwahi kutokea.

XS
SM
MD
LG