Mkutano huo unajiri wakati ambapo mivutano baina ya nchi hizo jirani inazidi kuongezeka.
Taarifa ya msemaji huyo serikali ya Tshisekedi imeeleza kwamba viongozi hao wawili watajadili mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo na uasi unaoendelea mashariki mwa Congo.
Muyaya amesema viongozi hao watatafuta suluhisho la kile amekitaja kuwa "uchokozi wa Rwanda nchini Congo." DRC imekuwa ikidai kuwa serikali ya Kigali inawaunga mkono wapiganaji wa kundi la M23 mashariki mwa nchi hiyo, lakini Rwanda imekuwa ikikanusha madai hayo.
Mkutano huo unafuatia ombi la Umoja wa Afrika kumtaka kiongozi wa Angola kuwa mpatanishi wa mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokasia ya Congo.