Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 21:09

Algeria kutoa pesa kwa wananchi wasiokuwa na ajira


Abdelmadjid Tebboune
Abdelmadjid Tebboune

Rais wa Algeria amesema serikali itaanzisha mpango wa kutoa pesa kwa watu wazima ambao hawana ajira, wakati nchi hiyo inakabiliwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.

Rais Abdelmadjid Tebboune amewaambia waandishi wa habari kwamba watu wanaotafuta ajira wenye umri wa miaka kati ya 19 na 40 wataanza kupewa pesa za matumizi kuanzia mwezi machi mwaka 2022.

Watapewa dola za Marekani 73 kwa mwezi pamoja na huduma ya afya hadi watakapopata ajira.

Wakati akitoa tangazo hilo Tebboune amesema kwamba Algeria itakuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya kutekeleza mpango kama huo.

Ameongea kwamba nchi hiyo ina zaidi ya watu 600,000 ambao hawana ajira.

XS
SM
MD
LG