Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 01:07

Algeria yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Morocco


Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune

Waziri wa mambo ya kigeni wa Algeria Ramtane Lamamra amesema Jumanne kwamba taifa lake limevunja uhusiano wa kidiplomasia na Morocco, wakati uhusiano kati ya mataifa mengi ya Afrika Kaskazini ukiendelea kudorora.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP Lamamra alisoma taarifa ya rais kuhusiana na hatua hiyo. Tangazo hilo limekuja baada ya karibu wiki moja tangu rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune kulieleza baraza la usalama kuhusu uchokozi wa Morocco, wakati akisisitiza umuhimu wa kutathmini tena uhusiano wa mataifa yote mawili, pamoja na haja ya kuimarisha usalama kwenye mpaka wao.

Algeria na Morocco kwa muda mrefu wameishi katika mazingira ya mivutano huku wakiwa wamefunga mipaka baina yao. Hali ilidorora zaidi wiki kadhaa zilizopita baada ya balozi wa Morocco kwenye Umoja wa Mataifa kusema kwamba watu wa Algeria kwenye eneo la Kabyle wanastahili kupewa nafasi ya kuamua hatima yao.

Algeria imekua ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Polisario ambalo linadai kujitawala kwa eneo hilo lililotekwa na Morocco mwaka 1975.Algeria pia imekuwa ikidai kwamba Morocco inaunga mkono kundi la wapiganaji kwenye eneo la Berber katika jimbo la Kabyle.

Wiki iliyopita Algeria ilidai kwamba mioto ya msituni iliyoshuhudiwa nchini humo ilianzishwa na makundi ya kigaidi, ambayo yanaungwa mkono na Morocco. Mioto hiyo ilianza Agosti 9, na inasemekana kuteketeza maelfu ya hekari wakati ikisababisha vifo vya takriban watu 90 wakiwemo wanajeshi 30.

XS
SM
MD
LG