Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:14

Algeria yasitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Morocco


Bendera ya Algeria
Bendera ya Algeria

Algeria imesitisha usafirishaji wa mafuta nje ya nchi kupitia nchi Jirani ya Morocco kutokana na mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Taarifa kutoka ofisi ya rais wa Algeria imesema kwamba hatua hiyo imechukuliwa kutokana na vitendo vya Morocco visivyoheshimu umoja wa kitaifa wa Algeria.

Algeria inaishutumu Morocco kwa kuunga mkono makundi ya wanaotaka kujitenga ya Algeria.

Taarifa inasema kwamba rais wa Algeria ameiamuru kampuni ya mafuta ya Sonatrach kusitisha uhusiano wake wa kibiashara na kampuni ya umeme ya Morocco.

Bomba la mafuta kutoka Morocco hadi ulaya, linasafirisha gesi ya asili hadi Spain kupitia Morocco.

Serikali ya Morocco hupokea malipo kwa sababu bomba hilo linapita nchini mwake.

Morocco vile vile hutumia sehemu ya mafuta hayo kuzalisha asilimia 10 ya umeme.

Maafisa wa Algeria wamekataa kusaini mkataba mpya na Morocco. Mkataba wa awali ulifikia hatima yake jumapili.

Kampuni ya Sonatrach itaendelea kusafirisha mafuta hadi Spain kwa kutumia bomba la Medgaz.

XS
SM
MD
LG