Vyanzo vya habari nchini humo vimesema ajali hiyo ilitokea saa kumi na mbili na robo majira ya asubuhi Jumatano.
Treni ya mizigo iliyokuwa ikitoka Kazuramimba, ilikuwa inaelekea Kigoma Mjini.
Basi hilo ambalo ni mali ya kampuni ya Prince hamida iligonga treni ikitokea Kigoma Mjini kwenda Tabora.
Rais wa Tanzania John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu. Pia amewataka wadau wote wa usalama barabarani kuchukua hatua kudhibiti ajali hizo.