Wizara hiyo imeeleza kwamba basi hilo, lililokuwa likitoka mjini Cairo, liligonga lori lililobeba saruji, ambalo lilikuwa limeegeshwa, baada ya kupata hitilafu, katika jimbo la Assiut, takriban kilomita 370 kusini mwa mji huo.
Afisi ya gavana wa jimbo hili, ilisema kuwa basi hilo lilitekekea kwa haraka, na ilikuwa ni vigumu kwa waopoaji, kuondoa miili iliyokwama mle.
Shirika la Habari la Reuters limesema kuwa ubovu wa barabara na uendeshaji holela wa magari, ni kati ya sababu kuu za ajali za mara kwa mara nchini Misri, ambazo zimesababisha vifo vya darazoni za watu katika siku za karibuni.
Mwezi jana, watu 18 walipoteza Maisha yao, baada ya basi ndogo walimokuwa, kugongana na lori, kwenye jimbo la Giza, takribana kilomita 80 kutoka mjini Cairo.