Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 04:44

Misri yaishikilia meli ya Ever Green mpaka itakapo lipa fidia


Meli ya Ever Given

Misri itaishikilia meli kubwa ya makontena iliyofunga njia ya mfereji wa Suez mwezi uliyopita hadi pale mmiliki wake atakapo lipa fidia ya dola milioni 900.

Mmoja wapo ya makampuni ya bima za Meli, Ever Given ya Uingereza UK Club, imesema mamlaka ya mfereji wa Suez ilikataa pendekezo la kumaliza madai hayo ya fidia.

Inaeleza kwamba madai hayo ambayo ni pamoja na gharama za dola milioni 300 za ziada za kuiokoa meli na milioni 300 kwa ajili ya kupoteza sifa zake ni nyingi sana na kwa sehemu kubwa hazina msingi.

Ever Given imetia nanga katika ziwa Great Biotter katikati ya njia ya mfereji huo.

Meli hiyo yenye urefu wa mita 400 iligonga mwamba na kwenda upande hapo march 23 na kuondolewa baada ya siku sitakufuatia kazi kubwa ya kuchimba na kuisukuma.

zaidi ya meli 400 zililazimika kusubiri kupita kwenye mfereji huo wenye urefu wa km 193 unaounganisha bahari za Sham na Mediterranean.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG