Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 00:49

Afrika Kusini yatwaa ubingwa wa dunia mashindano ya vijana Kenya


Mmoja wa washindi wa mashindano ya IAAF Makala ya kumi

Afrika Kusini imetawazwa bingwa mpya wa dunia katika mashindano ya vijana walio na umri chini ya miaka 18, yaliyokamilika Jumapili jioni katika mji wa Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA timu ya Afrika Kusini iliibuka mshindi kwa kuzoa nishani 5 za dhahabu na fedha 3 na shaba 3, mbele ya mataifa zaidi ya 100 yaliyoshirki mashindano hayo ya IAAF makala ya kumi.

China ilimaliza katika nafasi ya pili kwa kuzoa nishani 5 pia za dhahabu, fedha 2 na shaba 4, ikifuatiwa na Cuba iliyozoa dhahabu 5 na fedha 2 na shaba moja.

Wenyeji Kenya waliambulia nafasi ya nne kwa kushinda jumla ya medali 15 zikiwapo dhahabu 4, fedha 7 na shaba 4 mbele ya Ethiopia ambayo ilipata dhahabu 4 na fedha 3 na shaba 5 na kumaliza ya tano.

Kenya ndio timu bora zaidi kutoka eneo la Afrika Mashariki na ndio ya pili barani Afrika nyuma ya Afrika Kusini, huku Ethiopia ikishikilia nafasi ya tatu barani Afrika.

Mataifa mengine katika orodha ya 10 bora ni; Urerumani iliyopata dhahabu 3, Jamaica iliyopata dhahabu 3, Ufaransa dhahabu 2, Ukraine dhahabu 2, na Uturuki iliyofunga oridha ya timu kumi bora ikiwa na dhahabu moja na fedha moja na shaba moja.

Mataifa mengine ambayo angalau kila moja lilipata dhahabu ni Uhispania, Ecuador, Brazil, na Jamhuri ya Czech.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Josephat Kioko, Kenya

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG