Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:22

AfDB yatabiri uchumi wa Bara la Afrika kukua kwa haraka zaidi


Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huko Abidjan, Ivory Coast, Sept. 16, 2016.
Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huko Abidjan, Ivory Coast, Sept. 16, 2016.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inasema uchumi wa bara hilo  unatarajiwa  kukua  kwa haraka zaidi  kuliko makadirio ya ulimwengu, lakini nakisi katika bajeti na biashara zitaendelea kuzielemea nchi nyingi wakati hatari zinaendelea.

Katika ripoti yake ya Macroeonomic Performance and Outlook kwa Afrika, iliyotolewa Alhamisi, AfDB imesema kiwango cha ukuaji wa pato la ndani (GDP) kimepungua hadi asilimia 3.8 mwaka 2022. Inatarajiwa pato hilo litaimarika na kufikia asilimia nne mwaka huu, ripoti hiyo imesema.

Kuboreka kwa uchumi, ambao bara hilo utaushuhudia kiwango cha ukuaji kitavuka matarajio ya kimataifa ya asilimia 2.7, “ inaashiria kuendelea kusimamia sera huko Afrika na jitihada za kimataifa za kupunguza athari zinazotokana na mishtuko ya nje na ongezeko la ukosefu wa uhakika wa kiuchumi na athari zinazotokana na matukio ya nje ya nchi” mkopeshaji wa bara hilo alisema.

Rais wa AfDB, Akinwumi Adesina amesema kuwa ufufuaji huu na uimarishaji wa uchumi wa bara la Afrika, hata hivyo unatokana na uchukuaji wa “tahadhari ya kuwepo matumaini” wakati kuna vikwazo kadhaa vinavyo yakabili masoko yanayoibuka duniani.

Hali ya kifedha duniani imekuwa ngumu na inakadiriwa kuendelea hivyo kwa kipindi kijacho, imechangiwa na ongezeko la hali tete katika masoko ya kimataifa ya fedha na kuendelea kuyumba kwa usambazaji wa mahitaji ya kimataifa,”Dk Adesina alisema. Lakini viwango vya juu vya riba katika upeo wa kimataifa vinasalia kuwa hatari mno kwa uchumi wa Afrika kwa kipindi kijacho.

Hasara na uharibifu unaotokana na matukio mabaya ya hali ya hewa kama vile ukame, vimbunga na mafuriko, pia yanaendelea kuwa tishio kubwa katika uimarishaji wa uchumi barani Afrika.

Hatari nyingine, kulingana na mtazamo huo, ni pamoja na utegemezi wa mauzo ya nje ya bidhaa, migogoro ya kikanda katika “ maeneo muhimu na hatari kama vile Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Mali, na Msumbiji” na vihatarishi vya kisiasa vinavyotokana na chaguzi kuu zinazotarajiwa kufanyika katika nchi kadhaa.

Habari hii imechapishwa na gazeti la " The East Africa"

XS
SM
MD
LG