Maafisa wa polisi walionekana wakiwaondoa watu kutoka kwa magari yaliyokwama huku kukiwa na dhoruba ya theluji katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Xinjiang.
Maeneo kadhaa ya China yanakabiliana na hali ya baridi kali huku watu wakirejea kutoka kwa sherehe za wiki moja za mwaka mpya wa China, huku theluji kubwa ikinyesha katika mji wa kaskazini mashariki wa Shenyang.
Maafisa wa idara ya taifa ya hali ya hewa walitoa onyo la hali ya hewa ya baridi kali hadi kiwango chake cha pili cha juu, gazeti la Global Times lilisema, huku theluji nyingi ikitarajiwa kote nchini hadi Alhamisi (Februari 22).
Forum