Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 10, 2025 Local time: 22:38

Kituo cha utafiti cha China, Antantika chazua wasiwasi


Uzinduzi wa China, wa kituo kipya cha utafiti wa kisayansi katika huko Antaktika, wiki iliyopita kumeibua mjadala kuhusu madhumuni na athari za upanuzi wa haraka wa uwepo wa China kwenye bara hilo.

Kikiwa kwenye Kisiwa kisichoelezeka karibu na bahari ya Ross, kituo cha Qinling ni kituo cha tano cha kisayansi cha China na kituo cha tatu cha utafiti katika bara hilo ambacho kinaweza kufanya kazi mwaka mzima.

Kituo hicho kina ukubwa wa mita za mraba 5,244 na kinaweza kukaliwa na hadi watu 80 wakati wa miezi ya kiangazi, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya China CGTN.

Kituo cha Qinling, kipo karibu na kituo cha McMurdo cha Marekani na kusini mwa Australia na ripoti ya kituo cha mafunzo ya kimkakati na kimataifa iliyochapishwa Aprili mwaka jana ilisema kinaweza kuruhusu China kukusanya taarifa za kijasusi kutoka kwa washirika wa Marekani, Australia na New Zealand.

Forum

XS
SM
MD
LG