Ujumbe wake kwenye mtandao wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter, ulikuja siku moja baada timu yake kusema kuwa imefanikiwa kumpata, baada ya wiki kadhaa za kutoweza kumfikia.
Navalny alikuwa anashikiliwa katika eneo la Vladimir mashariki mwa Moscow, na sasa yupo mjini Kharp, katika eneo la Yamal-Nenets, ambalo hushuhudia majira ya baridi kali. Navalny aliandika kwamba alisafirishwa "kwa tahadhari na kwa njia ya ajabu" kiasi kwamba, hakutarajia kwamba watu wangejua alikohamishiwa hadi Januari mwakani.
Mkosoaji huyo mkubwa wa seikali ya Vladmir Putin alikamatwa mwaka 2021 baada ya kurejea kutoka Ujerumani ambako alikuwa anaendelea kupata nafuu kutokana na kupewa sumu ya mishipa, tukio ambali aliilaumu Kremlin. Amekanusha mashtaka yote dhidi yake na kudai kwamba yamechochewa kisiasa.
Forum