Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 18:13

Navalny afunguliwa mashitaka mapya na Russia.


Kiongozi wa upinzani wa Russia Elexei Navalny akiwa na mawakili wake kwenye mahakama ya Moscow City Jumatatu. Picha ya video
Kiongozi wa upinzani wa Russia Elexei Navalny akiwa na mawakili wake kwenye mahakama ya Moscow City Jumatatu. Picha ya video

Mahakama ya Russia Jumatatu imemfungulia mashitaka mapya kiongozi wa upinzani aliyeko kizuizini Alexei Navalny, ambayo huenda yakamsababisha kubaki jela kwa miongo kadhaa.

Kesi hiyo mpya imeanza kwenye jela yenye ulinzi mkali huko Melekhovo, takriban kilomita 250 mashariki mwa Moscow ambako Navalny anatumikia kifungo cha miaka 9 jela kufuatia kupatikana na hatua ya udanganyifu na kuidharau mahakama.

Wanahabari hata hivyo hawakuruhusiwa kwenye ukumbi wa mahakama ya Moscow City, na badala yake walifuatilia yaliyokuwa yakiendelea, kwenye chumba tofauti kwa njia ya video.

Navalny mwenye umri wa miaka 47 alikamatwa Januari 2021 baada ya kurejea Moscow baada ya kumaliza matibabu nchini Ujerumani kufuatia madai ya kupewa sumu na utawala wa Russia.

Hapo awali alikuwa ameitisha maandamano dhidi ya utawala wa Kremlin baada ya kufichua ufisadi uliyokuwa unaendelea.

Forum

XS
SM
MD
LG